Bruno Fernandes atua Old Trafford

Manchester United imekamilisha dili la kumsajili kiungo mshambuliaji wa Sporting CP Lisbon Bruno Fernandes kwa kandarasi ya miaka mitano na nusu.

Bruno, 25, amejiunga na Manchester United kwa dau la paundi milioni 55 huku kukiwa na ongezeko la paundi milioni 47 hapo baadae.

“Nitajitaidi kufanya niwezavyo kurejesha mataji yaliyopotea klabuni hapa.”

“Kucheza hapa(Manchester United) ni ndoto ya kila mchezaji hata historia yake inaonyesha kuwa ni timu kubwa Ulaya”. Amesema Bruno Fernandes ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ureno.

“Mapenzi yangu katika timu hii yalianza zamani kidogo hasa wakati ule nikimtazama Cristiano Ronaldo tangu kipindi hicho nimekuwa shabiki mkubwa wa Manchester United” Aliongeza Bruno ambaye atasalia klabuni mpaka 2025.

Aidha, Ole Gunnar Solskjaer amesema kiungo huyo ni ongezeko bora katika kikosi cha United.

Usajili wa Fernandes umetokea mwezi Januari kuelekea kufungwa kwa dirisha dogo hili akiwa mchezaji wa kwanza msimu huu. Bruno anaungana na mastaa wengine kama Cristiano Ronaldo, Marcos Rojo, Luis Nani kujiunga na Manchester United kutokea Sporting.

Author: Bruce Amani