Bundesliga kuanza tena kutimua vumbi mwezi Mei?

Kuendelea kwa marufuku ya mikusanyiko mikubwa nchini Ujerumani hadi hapo mwezi Agosti mwaka huu kutokana na mripuko wa virusi vya corona kumewathiri viongozi wa soka nchini humu waliokuwa wakilenga kurejesha michezo ya ligi mnamo mwezi Mei bila ya kuwepo mashabiki uwanjani.

Tangazo lililotolewa Alhamisi hii na kansela wa Ujeruman Angela Merkel limesisitiza kutokuwepo na mikusanyiko ya zaidi ya watu 2 katika maeneo ya umma kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya mripuko wa virusi hatari vya Corona vinavyoendelea kuitesa dunia huku tangazo hilo likihakikisha msimu ujao wa ligi ya Bundesliga hautaanza kama ilivyokuwa imepangwa kuanza mwezi Agosti mwaka huu.

Baada ya mazungumzo kati ya kansela Merkel na magavana wa majimbo 16 yaliyokuwa yamelenga kulegeza vizuizi vilivyowekwa kwa ajili ya mapambano ya virusi vya Corona, Gavana wa Bavaria Markus Soder, alisema kuwa Bundealiga kwa sasa sio suala la muhimu kwa Sasa na kwamba kuna vipao mbele vikubwa muhimu zaidi ya soka.

Awali bodi ya ligi ya Bundesliga  DFL, ilitoa maelezo yenye mkanganyiko kwamba kila majimbo 16 nchini Ujerumani yanaweza kupanga namna mechi zake zitakavyochezwa. Kuna  uwezekano mkubwa wakatofautiana, ikimaanisha michezo mingine inaweza kuruhusiwa na wengine isiruhusiwe.

Rais wa Shirikisho la kandanda nchini Ujerumani, Fritz Keller anatarajia soka la Ujerumani kuanguka kwa muda.”Sidhani mazingira ya soka yatakuwa sawa kumalizika kwa mripuko wa janga la virusi vya Corona,” alisema Keller wiki iliyopita ma kuongeza kuwa,” tunakwenda kuvikosa baadhi ya vilabu, na ninafikiria kwamba kwa jinsi hali inavyoendelea, ndivyo tunakwenda kukabiliana na tatizo la kifedha katika soka la Ujerumani.

Vilabu vya soka vya Paderboen pamoja na Schalke katika ligi ya Bundealiga vimeripotiwa kukabiliwa na mdororo wa kiuchumi wakati jarida la Kicker la hapa Ujerumani limesema kuwa vilabu 13 katika ligi daraja la pili nchini humu pia vinakabiliwa na tishio kama kutacheleweshwa kwa malipo ya utangulizi ya fedha kwa DFL kutokana na haki za matangazo ya televisheni.

“Tunaweza kumudu mwezi mmoja au miwili ijayo, lakini badae hatutakuwa hewani.”Mkurugenzi mtendaji wa Paderboen Martin Przondziono alimuambia mtangazaji wa Sport1 na kuongeza kuwa kama pesa za matangazo ya televisheni hazitatolewa itakuwa ni ngumu kwetu sisi.”

Timu ya Schalke haijaficha matatizo ya kifedha iliyonayo yaliyosabanishwa na mripuko wa virusi vya corona licha ya maandalizi ya udhamini na kampuni kubwa ya nishati ya Gazprom wenye thamani ya euro milioni 30 kwa kila msimu

Mkurugenzi wa mawasiliano wa timu hiyo, Alexander Jobst mwezi uliopita aliuliza wamiliki wa masanduku kwenye uwanja ili kuondoa ulipaji wa sehemu kwa michezo yake ya mwisho ya nyumbani.

Naye mkurugenzi wa fedha wa klabu ya Schalke Peter Peters, wiki hii aliwaonya mashabiki wa klabu hiyo kwamba hali ya Klabu hiyo ilikuwa hatarini.”Tunajaribu kupunguza gharama, tumepunguza masaa ya kufanya kazi kwa waajiriwana tumekubaliana kupunguza mishahara yabwachezaji,” alisema Peters katika mtandao wa facebook na kuongeza kuwa,”lakini bila shaka kila kitu kitategemea na ni lini tutapata pesa na kucheza soka tena soka.”

Vilabu vya Bundealiga vitakutana tena April tarehe 23 kwa ajili ya kujadili ni kwa namna gani vitakavyomaliza maimu wa ligi hiyo Kama ilivyokuwa imepangwa kufikia June 30.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends