Bundesliga yarejea! Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kandanda linaweza kurejea katikati ya Mei

Kandanda limerudi!

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wa majimbo yote 16 ya Ujerumani wametoa idhini kwa ligi kuu ya kandanda Ujerumani Bundesliga kuumalizia msimu huu bila mashabiki viwnjani kuanzia katikati ya Mei baada ya wiki kadhaa za kusitishwa kutokana na hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Baraka hiyo ya kisiasa inaifanya ligi kuu ya Ujerumani kuwa ya kwanza kati ya tano kuu za Ulaya kurejea dimbani. “mechi zitaruhusiwa chini ya kanuni zilizoidhinishwa,” alisema Merkel katika kikao cha wanahabari mjini Berlin. Viongozi hao wameidhinisha mpango uliowasilishwa na DFL wa kurejea Bundesliga katika viwanja vitupu n wachezaji kufanyiwa vipimo vya mara kwa mara.

DFL sasa lazima iweke tarehe ya kurejea michuano ambapo huenda ikawa Mei 16 au 17 au wikendi inayofuata.

“Uamuzi wa leo ni habari njema kwa Bundesliga,” amesema Afisa Mkuu Mtendaji Christian Seifert.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends