Bundesliga yatafakari wachezaji zaidi wa akiba

Vilabu vya ligi kuu ya Kandanda Ujerumani – Bundesliga vitaruhusiwa kuongeza wachezaji wawili zaidi kwenye benchi la wachezaji wa akiba kuanzia msimu ujao katika pendekezo lililowasilishwa na maafisa wa kandanda

Kamati ya Kitengo kinachosimamia ligi za daraja ya kwanza na ya pili Ujerumani – DFL imeunga mkono timu kuwa na wachezaji tisa badala ya saba kwenye benchi la akiba, ijapokuwa ni wachezaji wasiozidi watatu pekee ndio watakaoendelea kuruhisiwa kuingia uwanjani kama nguvu mpya. Pendekezo hilo la kamati kuu ya DFL litahitaji kuidhinishwa na bodi inayosimamia ligi hiyo.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Ujerumani, DFB Pokal, sasa inakubaliwa mchezaji wa nne kuingia kama nguvu mpya wakati wa kipindi chochote cha muda wa ziada.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends