Bye Bye Simba, Francis Kahata awaaga mashabiki wa Simba

Sasa ni rasmi mchezaji “kijiko” ndani ya Simba Francis Kahata amejiweka kando na Wekundu wa Msimbazi.

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya ambaye amewai kusakata kabumbu ndani ya Gor Mahia Francis Kahata amewaaga mashabiki na viongozi wa Simba kufuatia kandarasi yake kumalizika klabuni hapo.
Akufukuzaye hakuambii toka! Kahata jina lake lilitolewa kwenye orodha ya nyota watakaoshiriki Ligi Kuu Bara na kuwa kwenye orodha ya wachezaji Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo nafasi yake ilichukuliwa na kiungo Perfect Chikwende.
Baada ya timu ya Simba kuishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dili la Kahata likawa limeisha na mabosi wa Simba hawakuwa na mpango wa kumuongezea dili jingine, akaamua kung’oka mazima.
Kahata ameandika kwenye Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kiwa “Asanteni Wanasimba kwa sapoti, benchi la ufundi pamoja na wachezaji, najivunia muda wangu ndani ya timu hii na mafanikio niliyoyapata.
“Ilikuwa safari yenye kumbukumbu tamu na chungu. Ni wakati wa kutafuta changamoto nyingine, asanteni, mpaka wakati mwingine”.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares