CAF haijafikia uamuzi kuhusu Ivory Coast kuandaa AFCON 2023

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limesema halijafikia uamuzi wowote wa kuipa nafasi Ivory Coast kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la Afrika mwaka 2023 badala ya 2021.

Kauli hii ya CAF imekuja baada ya rais wa Shirikisho hilo Ahmad Ahmad kunukuliwa akisema kuwa Cameroon imepewa nafasi ya kuwa mwenyeji mwaka 2021. Camerron iliondolewa uwenyeji wa kuandaa fainali za mwaka 2019, kwa sababu ya maandalizi mabaya lakini pia suala la usalama. Ivory Coast imekwenda katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo, kupinga uwezekano wowote wa kupokonywa haki za kuandaa fainaliza mwaka 2021.

Wakati uo huo, mwenyeji wa AFCON mwaka 2019, anatarajiwa kutajwa tarehe 9 mwezi Januari 2019. Misri na Afrika Kusini zimethibitisha kuwa mwenyeji wa fainali hiyo itakayofanyika kayi ya mwezi Juni na Julai na kwa mara ya kwanza, mataifa 24 yanatarajiwa kushiriki.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments