CAF kuamua Januari 9 mwenyeji wa AFCON 2019

Afrika Kusini huenda ikaiingilia kati na kuwa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2019. Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Kandanda Afrika –CAF Ahmad Ahmad katika mahojiano na shirika la habari la AFP.

CAF imekuwa ikifanya tathmini kuhusu suluhisho mbadala la kuandaa tamasha hilo la Juni 15 hadi Julai 13 baada ya Cameroon kuvuliwa uwenyeji kutokana na kucheleweshwa kwa matayarisho na wasiwasi wa usalama.

Ahmed amesema uamuzi wa mwisho wa nani ataandaa kinyanganyiro hicho cha kandanda mwaka ujao utatangazwa Januari 9.

Ameongeza kuwa kwa sasa kuna nchi mbili au tatu ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kuchukua mikoba ya Cameroon, akiitaja Afrika Kusini kuwa nchi iliyowasilisha barua ya nia ya kuandaa. “kwa mujibu wa habari nilizo nazo, barua mbili au tatu za nia ya kuwa mwenyeji zimewasili” alisema rais huyo wa CAF raa wa Madagascar.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments