CAF yaahirisha droo ya michuano ya vilabu msimu ujao

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limesema limeahirisha droo ya michuano ya kutafuta ubingwa klabu bingwa na Shirikisho msimu 2019 kwa sababu maalum.

Droo hiyo ilitarajiwa kufanyika mjini Rabat nchini Morocco, Jumapili iliyopita.

Duru zinasema kuwa droo hiyo iliahirishwa kwa sababu klabu za Morocco kuleta mkanganyiko kuhusu namna droo hiyo itakavyokuwa, kwa timu zake zinazocheza katika michuano ya kuwania taj la Shirikisho.

Klabu ya Hassania Agadir, Renaissance Berkane au Wydad Fes zote zinaelezwa kuwa zimefuzu kucheza fainali ya Shirikisho lakini pia iwapo Raja Casablanca itashinda fainali ya mwaka huu ya taji la Shirikisho, itafuzu pia.

Casabalanca inacheza nyumbani na ugenini dhidi ya AS Vita Club ya DRC, katika fainali hiyo. Kanuni za CAF, haziruhusu klabu tatu kucheza katika mashindano ya kuwania taji moja, na iwapo Raja Casablanca watashinda mechi hiyo, klabu ya Hassania itabidi iondoke kwenye mashindano hayo.

Mashindano ya mwaka huu yanatarajiwa kuanza tarehe 27 mwezi Novemba na kumalizika tarehe 1 mwezi Juni mwaka 2019.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends