CAF yaridhishwa na hatua za kudhibiti maambukizi ya corona michezoni

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limesema utaratibu wa kiafaya uliowekwa katika mechi za wiki hii na wiki iliyopita, kufuzu kucheza fainali ya Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon, ulifuatwa kikamilifu, wakati huu bara la Afrika na dunia, inapoendelea kukabiliwa na janga la Corona. CAF imesema mechi zote 48 za kufuzu zilichezwa katika viwanja mbalimbali barani Afrika. Kati ya wachezaji na maafisa zaidi ya Elfu nne waliopimwa maambukizi ya Corona, ni 48 ndio waliopatikana kuambukizwa. Hadi sasa mataifa manne yameshafuzu katika faninali hizo na ni pamoja na Algeria, Senegal, Mali na Tunisia.

Author: Kaka Abuso