Camavinga amwaga wino miaka sita Real Madrid

Real Madrid imekamilisha uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa na Rennes Eduardo Camavinga kwa mkataba wa miaka sita kutumika klabuni hapo.

Camavinga mwenye umri wa miaka 18, anatajwa kuwa kipaji cha hali ya juu ambapo mkataba wake ulikuwa umeingia kwenye mwaka wa mwisho, na klabu yake haikuwa tayari kumpoteza huru mwishoni mwa msimu huu.

Alikamilisha vipimo vya afya Ufaransa siku ya Jumatatu, ambapo pia mwaka 2019 mwezi Aprili Camavinga alikuwa mchezaji mdogo miaka 16 kucheza mechi ngazi ya taifa.

Katika misimu miwili iliyopita, Eduardo Camavinga amecheza jumla ya mechi 60.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares