Cameroon yaanza vyema kampeni ya kutetea ubingwa Afcon

140

Mabingwa watetezi wa mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON Cameroon wameanza vizuri kwenye michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Guinea-Bissau.

Cameroon ikiwa na utofauti mkubwa kwenye michuano ya mwaka huu hasa mara baada ya msimu uliopita kutumia vijana lakini mambo mwaka huu ni tofauti kidogo.

Ushindi wa Cameroon umepatikana kupitia magoli ya haraka ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Yaya Banana kunako dakika ya 66 kabla ya Stephane BAHOKEN kumalizia sherehe ya mabingwa hao kunako dakika ya 68.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Cameroon kuwa vinara wa kundi F baada ya kujikusanyia alama tatu, Guinea-Bissau alama sifuri wakati ambao Ghana na Benin watacheza leo baadae kukamilisha ratiba ya michuano ya AFCON 2019 kwa raundi ya kwanza.

Mchezo wa Ghana dhidi ya Guinea-Bissau utakamilisha ratiba ya mkondo wa kwanza kwa mashindano haya

Author: Bruce Amani