“Ghost” arejea tena kama kocha wa Harambee Stars

Shirikisho la Kandanda Kenya –FKF limemtambulisha Jacob “Ghost” Mulee kuchukua usukani wa timu ya taifa ya kandanda ya Harambee Stars. Mulee ametangazwa saa chache tu baada ya kocha Francis Kimanzi kujiuzulu. Mulee anarudi usukani baada ya kuiongoza Harambee Stars katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2004 iliyoandaliwa Tunisia: Kimanzi na wasaidizi wake wawili

Continue Reading →

Drogba ajitosa kinyang’anyiro cha rais wa chama cha soka Ivory Coast

Nguli wa kandanda aliyewapa burudani mashabiki wa Chelsea dimbani Stamford Bridge Didier Drogba amejitosa rasi katika kinyang’anyiro cha Urais wa chama cha soka cha Ivory Coast. Drogba mwenye umri wa miaka 42, ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Afrika ni miongoni mwa wagombea wanne wanaotafuta ridhaa ya kukiongoza chama cha soka katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Hata hivyo, hana uhakika iwapo atashiriki katika uchaguzi huo uliopangwa Septemba 5. Pamoja na kuhitaji uteuzi kutoka kwa vitatu kati ya vilabu 14 vya ligi kuu ya Ivory Coast na viwili kutoka ligi

Continue Reading →

Mauritius yaingia makubaliano na Liverpool katika zoezi la ukuzaji soka na kutangaza vivutio

Maendeleo ya mpira wa miguu yanahitaji ushirikiano baina ya watu, nchi, na taasisi ambazo zimepiga hatua katika sayansi ya soka katika ngazi tofauti tofauti. Mataifa ambayo yameendelea kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya timu za wakubwa na timu zote za wadogo lakini mataifa ambayo yanachipukia mfumo huo umekuwa changamoto kubwa kufuatwa kutokana na

Continue Reading →