Marefarii wapewa mafunzo na CAF

Zaidi ya marefarii 40 wa mchezo wa soka kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wamemaliza mafunzo yaliokuwa yanatolewa na Shirikisho la soka Afrika – CAF. Mafunzo hayo yaliwaleta pamoja marefarii wachanga waliopimwa afya na kufanya mazoezi ya kimwili katika uwanja wa soka wa Namboole nchini Uganda. Moses Magogo Rais wa Shirikisho la soka Uganda – FUFA

Continue Reading →

Gor Mahia yapigwa faini na CAF

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF, imeitaka klabu ya Gor Mahia nchini Kenya, kulipa faini ya Dola 5,000 baada ya mashabiki wa klabu hiyo kuzua fujo wakati wa mechi ya hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda. Mechi hiyo ilichezwa mwezi Agosti katika uwanja wa

Continue Reading →

Esperance yaizima Etoile Sahel

Uhaba wa mabao katika robo fainali ya dimba la Ligi ya Klabu bingwa Afrika – CAF Champions League ulikamilika katika mchuano wa mwisho wakati Esperance iliipiku Etoile Sahel 2-1 katika mchuano wa mkondo wa kwanza kati ya vilabu hivyo viwili vya Tunisia. Katika mechi nyingine ya robo fainali, mapambano kati ya Primeiro Agosto ya Angola

Continue Reading →

Rayon yaiteka Enyimba mjini Kigali

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika – CAF Confederation Cup, kipa wa Enyimba Theophilus Afelokhai aliendeleza hali yake bora ya mashindano hayo kwa kuyazima mashambulizi ya Rayon Sports ya Rwanda katika sare yao ya 0-0 mjini Kigali. Katika matokeo mengne, Raja Casablanca ya Morocco iliweka guu moja kwenye nusu fainali baada ya kuibamiza

Continue Reading →

Michuano ya robo fainali ya CAF yaanza

Michuano ya hatua ya robo fainali, kuwania Kombe la klabu bingwa – CAF Champions League na Shirikisho barani Afrika – CAF Confederation Cup, inachezwa mwishoni mwa juma hili. Ijumaa usiku, Horoya ya Guinea itakuwa nyumbani kucheza na Al Ahly ya Misri huku ES Setif ikimenyana na Wydad Casablanca ya Morocco. Jumamosi kuanzia saa saa moja

Continue Reading →

Maafisa wa FERWAFA wachunguzwa kwa rushwa

Maafisa wawili wa Shirikisho la Kandanda la Rwanda – FERWAFA wanafanyiwa uchunguzi na Shirika la Upelelezi la Rwanda – RIB, kuhusiana na tuhuma za kashfa ya rushwa inayomhusisha refarii. Maafisa wa RIB wamesema kuwa Katibu Mkuu wa FERWAFA Francois Regis Uwayezu na Kamishna wa Mashindano Eric Ruhumiriza walitiwa nguvuni Alhamisi Septemba 12. Kashfa hiyo iligonga

Continue Reading →

Manishimwe aurefusha mkataba na Rayon Sports

Kiungo wa klabu ya Rayon Sports ya Rwanda, Djabel Manishimwe ameongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi wa kuichezea klabu hiyo. Taarifa ya mchezaji huyo kuongeza mkataba mpya imetolewa na Bernard Itangishaka ambapo kwa sasa mchezaji huyo atasalia hadi mwaka 2020. Manishiwe alijiunga na Rayon Sports mwaka 2014 akitokea klabu ya Isonga na amekuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha

Continue Reading →

Mwendwa kuwania wadhifa wa FIFA

Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya, FKF Nick Mwendwa atawania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka duniani Fifa baadaye mwezi huu akiwakilisha kanda ya nchi zinazozungumza lugha ya kiingereza. Awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka nchini Ghana, Kwesi Nyantakyi ambaye alijiuzulu kwa tuhuma za

Continue Reading →

Tunaweza kutisha Cameroon 2019

Pengine kwa mara ya kwanza mataifa ya Afrika Mashariki yamepata matokeo chanya katika michezo yake ya awali ya kuwania kufuzu kucheza kombe la mataifa ya Afrika nchini Cameroon mwakani. Tuanze na Kenya, Harambee Stars ikicheza nyumbani katika jiji la Nairobi iliwashangaza wapenzi wa soka wa Afrika kwa kuifunga Ghana ambayo ni moja ya kigogo cha

Continue Reading →

Weah arejea uwanjani dhidi ya Nigeria

Rais wa Liberia na mshindi wa zamani wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Ulimwenguni George Weah alirejea tena uwanjani katika mchuano wa kimataifa mjini Monrovia, lakini timu yake ilipata kipigo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya Nigeria. Mchuano huo ulikuja wiki chache tu kabla ya rais huyo kusherehekea miaka 52 ya kuzaliwa kwake.

Continue Reading →