Shirikisho la mchezo wa riadha duniani IAAF, limetangaza kuwa, kuanzia mwaka 2020, mashindano ya mbio za Mita 200 na 3,000 kuruka viunzi na maji, hayatajumuishwa katika mashindano ya Diamond League. Kila mwaka kuna mashindano 15 ya Diamond League na sasa mashindano 12 ya riadha ndio yatakoyosalia. IAAF inasema lengo ni kuwezesha mashindano hayo kusalia na
