Maafisa saba waandamizi nchini Kenya watashitakiwa kutokana na sakata la rushwa linalohusishwa Michezo ya Olimpiki ya 2016. Mwendesha mkuu wa mashitaka Noordin Haji amesema kuwa maafisa hao wanapaswa kujisalimisha kwa polisi ifikapo Jumatatu tarehe 15 Oktoba. Miongoni mwao ni waziri wa zamani wa michezo Hassan Wario ambaye sasa ni balozi wa Kenya nchini Austria na
