Dortmund yabanduliwa nje ya Kombe la DFB

Vinara wa ligi kuu ya Ujerumani, Borussia Dortmund wameondolewa kwenye michuano ya kombe la Ujerumani, baada ya kutandikwa 4-2 kupitia mikwaju ya penalti na Werder Bremen katika hatua ya 16 bora jana Jumanne. Dakika 120 za mchezo huo zilishuhudia timu hizo zikitoka sare ya mabao 3-3. Max Kruse aliifungia Bremen penalti ya ushindi huku mlinda

Continue Reading →

Bayern yashindwa kupunguza pengo dhidi ya Dortmund

Mabingwa watetezi Bayern Munich walibumburushwa kwa kufungwa 3-1 na Bayer Leverkusen siku ya Jumamosi na kuwaruhusu Borussia Dortmund kutanua uongozi wao kileleni mwa Bundesliga na pengo la pointi saba. Mabao ya kipindi cha pili ya wachezaji wa Leverkusen Leon Bailey, Kevin Volland na Lucas Alario yawalipa kichapo cha nne msimu huu Bayern ambao wanashikilia nafasi

Continue Reading →

Sandro Wagner aondoka Bayern na kuelekea China

Mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani Sandro Wagner amewaambia kwaheri mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich na kujiunga na klabu ya China Tianjin Teda. Vilabu vyote viwili vimethibitisha habari hiyo. Wagner aliyezaliwa Munich anaondoka Bayern baada ya mwaka mmoja kwa sababu hakuwa anapata nafasi nyingi za kucheza chini ya kocha Niko Kovac, na hakuwa kwenye kikosi kabisa

Continue Reading →

Bayern waanza mzunguko wa pili wa msimu na ushindi

Bayern Munich wameanza mzunguko wa pili wa msimu kwa kuonyesha mchezo imara na kuwazidi nguvu Hoffenheim kwa kuwafunga mabao sawa na walivyofanya katika siku ya kwanza ya msimu.   Timu hiyo ya kocha Niko Kovac iliutawala mchezo katika kipindi cha kwanza baada ya kupoteza nafasi kadhaa kabla ya Leon Goretzka kufunga. Robert Lewandowski alipiga kichwa

Continue Reading →

Bayern wamnyakua beki Mfaransa Pavard kutoka Stuttgart

Mabingwa wa Ujerumani kwenye ligi kuu ya Bundesliga Bayern Munich wamefanikiwa kumsajili mlinzi raia wa Ufaransa Benjamin Pavard akitokea Stuttgart ambao ni wapinzani wa Munich. Bayern wamesema Pavard, 22, atajiunga nao mwezi Julai baada ya kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia alipocheza michezo yote 6 ya timu yake ya Ufaransa. Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Hassan Salihamidzic amesema Pavard amesaini mkataba

Continue Reading →