Tangia Novemba 21, Borussia Dortmund ilikuwa haijafanikiwa kushinda mechi yoyote na bao la Marco Reus limeipa matokeo chanya katika mechi ya Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga kwa kuifunga Werder Bremen goli 2-1. Dortmund juzi ilitangaza kumfuta kazi kocha wake mkuu Lucien Favre baada ya kipigo cha goli 5-1 dhidi ya Stuttgart na ushindi huo umekuja
