Droo ya robo fainali Champions League yaweka uwezekano wa Bayern – Barcelona

Real Madrid huenda ikakutana na Juventus ya shujaa wao wa zamani Cristiano Ronaldo katika robo fainali ya Champions League wakati miamba ya Ujerumani huenda ikakutana na Barcelona. Droo iliyofanywa na Shirikisho la vyama vya kandanda Ulaya – UEFA imewapanga wageni wa mashindano hayo Atalanta dhidi ya Paris Saint-Germain na RB Leipzig na Atletico Madrid. Real kwanza

Continue Reading →

Msimu utafutwa kama mpango A, B na C utafeli – Rais wa Uefa Ceferin

Rais wa Uefa Aleksander Ceferin amesema msimu wa soka utafutwa kama utashindwa kuendelea mpaka mwishoni mwa mwezi Juni. Ligi mbalimbali Ulaya zimesimamishwa kutokana na janga la virusi vya Corona, ambapo mashindano ya Euro 2020 yaliyotakiwa kufanyika mwaka huu mwezi Juni yamehairishwa pia mpaka 2021. Ceferin amesema ligi zitaweza kumalizika hata kuchezwa bila uwepo wa mashabiki.

Continue Reading →

PSG yashinda dhidi ya Dortmund

Laana imekwisha. Ile laana iliyokuwa ikiitesa Paris St-Germain ya kutofanya vizuri katika mashindano ya Uefa hatimaye wameimaliza baada ya kubadilisha matokeo kutoka 2-1 mchezo wa kwanza mpaka 3-2 katika mtanange uliopigwa dimba la Parc des Princes dhidi ya Borussia Dortmund. Katika mtanange ambapo umepigwa bila uwepo wa mashabiki kutokana na hofu ya Virusi vya Corona,

Continue Reading →

Spurs ya Mourinho yatimuliwa na RB Leipzig

Klabu ya Tottenham Hotspurs ya kocha Jose Mourinho imeyaaga rasmi michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2019/20 kwa kuondolewa na RB Leipzig, licha ya msimu uliopita kufika hadi hatua ya fainali. Mourinho na vijana wake walikuwa ugenini Ujerumani lakini walienda kutafuta ushindi kwa kuwa mchezo wa kwanza nyumbani kwao London walipoteza mchezo huo kwa

Continue Reading →

Juventus hoi kwa Lyon, yalazwa 1 – 0

Mabingwa mara nane mfululizo wa Serie A Juventus wamekubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Lyon katika mchezo wa raundi ya kwanza hatua ya 16 bora ya Uefa kwenye mchezo uliopigwa nchini Ufaransa. Alikuwa ni Lucas Tousart ambaye aliitumia vyema krosi ya Houssem Aouar na kumalizia mpira uliokuwa zao goli pekee katika mchezo huo. Vinara

Continue Reading →

Chelsea yalala mbele ya Bayern Munich

Ndoto za Chelsea kufanya vizuri kwenye michuano ya Uefa huenda zimefikia tamati leo Jumanne baada ya kukubali kichapo cha goli 3-0 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora mkondo wa kwanza uliofanyika Stamford Bridge. Kinara huyo wa Bundesliga amefuata nyanyo za RB Leipzig kwa kucheza na timu

Continue Reading →

Klopp awatisha Atletico licha ya kushindwa

Jurgen Klopp amewaonya Atletico Madrid kuwa wasishangilie kuibuka na ushindi wa mchezo wa raundi ya kwanza ya Uefa champions league kana kwamba wameshacheza Anfield mkondo wa pili. Klopp amesema tumecheza kipindi kimoja Madrid bado dakika nyingine 45 za kipindi cha pili hivyo Atletico Madrid hawapaswi kuwa na furaha kiasi hicho. Kauli ya Klopp inakuja siku

Continue Reading →