Ratiba ya msimu mpya wa kandanda Kenya yatolewa

Kampuni inayosimamia ligi kuu ya soka nchini Kenya KPL, tayari imetangaza kuanza kwa msimu mpya wa ligi nchini humo. Kwa mara ya kwanza, ligi itaanza mwezi Desemba na sio Februari kam ilivyokuwa desturi. Msimu mpya utaanza tarehe nane mwezi Disemba ambapo mabingwa watetezi Gor Mahia wataanza harakati za kutetea taji lao dhidi ya Bandari FC

Continue Reading →

Sofapaka yalenga dimba la Afrika

Klabu ya Sofapaka itacheza kwenye soka la Bara Afrika, hayo hi matamshi ya kocha ya timu hio John Baraza ambaye anasema fainali ya tarehe 20 kati yao na Kariobangi Sharks itakuwa ya muhimu kuliko mechi nyinginezo walizowahi kushiriki. Sofapaka inalenga kurejea kwenye soka ya Afrika baada ya kushiriki mara ya kwanza mwaka 2009 walipolitwaa taji

Continue Reading →

Gor wakabidhiwa rasmi Kombe la KPL

Gor Mahia walinyanyua Kombe la Ligi Kuu ya Kandanda nchini Kenya kwa mara ya 17 katika sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Moi mjini Kisumu. Hata hivyo vijana hao wa kocha Dylan Kerr walilazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili na Mathare United licha ya kuwa wao ndio walikuwa kifua mbele 2-0 kupitia mabao

Continue Reading →

Batambuze kujiunga na Gor

Mchezaji wa kimataifa wa Uganda Shafik Batambuze anatarajiwa kujiunga na klabu ya Gor Mahia ya Kenya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu. Batambuze kwa sasa hana timu baada ya kuichezea Singida United ya Tanzania msimu uliopita. Mtendaji mkuu wa Gor Mahia Lodvick Aduda ameviambia vyombo vya habari nchini Kenya kwamba Batambuze na mchezaji

Continue Reading →

Chui wadai posho lasivyo waendelee kupoteza

Mzozo unatokota katika klabu ya AFC Leopards baada ya wachezaji kudaiwa kufanya mgomo baridi, wakidai posho kutokana na mechi tisa ambazo wameshinda katika mzunguko wa pili wa msimu wa Ligi Kuu ya Kandanda Kenya. Duru zinaarifu kuwa kila mchezaji anadai shilingi za Kenya karibu 70,000 kutoka kwa usimamizi wa klabu ikiwa ni marupurupu ya mechi

Continue Reading →

Agwanda mchezaji bora kwa mwezi wa pili mfululizo

Nahodha msaidizi wa Sony Sugar Enock Agwanda amekuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda mara mbili mfululizo tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ya Sportpesa/LG/SJAK, katika ligi kuu ya Kandadna nchini Kenya baada ya kunyakua tuzo hiyo kwa mwezi wa Agosti katika uwanja wa Awendo. Mchezaji huyo aliyewahi kuzichezea timu za Gor Mahia na Sofapaka alipata

Continue Reading →

Ulinzi yaibamiza Gor na kuipa kipigo cha nne mfululizo

Mfululizo wa matokeo mabaya ya Gor Mahia uliendelea Jumatano 19.09.2018 wakati waliposhindwa na Ulinzi Stars kwa mabao 2-0 katika mtanange wa ligi kuu ya kandanda nchini Kenya – KPL. Mchuano huo ulichezwa katika uwanja wa michezo wa Kaunti ya Machakos. Elvis Nandwa alikuwa mwiba katika safu ya ulinzi ya Gor alipofunga goli katika kila kipindi

Continue Reading →