Kikosi cha Barcelona kimefanikiwa kuibuka kidedea dhidi ya Sevilla katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga kwa ushindi wa goli 2-0 huku Lionel Messi akihusika katika bao zote mbili. Ushindi huo unaifanya Barca kuwa alama mbili nyuma ya vinara Atletico Madrid ambao bado wana michezo miwili mkononi. Messi alianza kutengeneza bao la winga
