Real Madrid wamekubali sare na kupoteza nafasi ya kushika usukani wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga baada ya kutoa sare tasa dhidi ya Osasuna katika mchezo uliopigwa Jana Jumamosi. Kabla ya kuchezwa kwa mechi hiyo kulikuwa na hofu ya kuwa huenda mtanange huo usingechezwa kutokana na hali ya hewa kutokuwa rafiki lakini baadae ukaruhusiwa
