Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino amekiongoza kikosi chake kupunguza pengo la alama hadi tatu kileleni baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Marseille mtanange uliopigwa Jana Jumapili. Kylian Mbappe na Mauro Icardi walifunga goli moja moja katika kipindi cha kwanza kwa upande wa mabingwa hao watetezi wa Ligue 1 ambao bado wanabakia nafasi ya tatu.
