Toby Alderweireld ang’oka Spurs

Klabu ya Tottenham Hotspur imefikia maamuzi ya kumuuza mlinzi wake wa kati raia wa Ubeligiji Toby Alderweireld kwenda klabu ya Al-Duhail ya Qatar. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, aliyejiunga na Spurs mwaka 2015, amesafiri mpaka Jijini Doha na inaelezwa kuwa utambulisho wake unategemewa kufanyika wiki ijayo. Toby anaondoka klabuni hapo baada ya mechi

Continue Reading →

Telles wa Man United kukosa mechi za mwanzoni mwa msimu

Mlinzi wa pembeni wa Manchester United Alex Telles atakosa mechi ya mwanzoni mwa msimu ujao kufuatia majeruhi ya enka ambayo aliyapata kwenye mazoezi wiki iliyopita. Telles, 28, anaweza kukosa mechi za mwanzoni ambazo ni dhidi ya Leeds, Southampton na Wolves. Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa walitegemea kuwa angerudi uwanjani mapema lakini mambo

Continue Reading →

Solskjaer amwaga wino kuendelea kutumika Man United

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesaini mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho mpaka mwaka 2024 kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine.   Kocha huyo raia wa Norwei mwenye umri wa miaka 48, aliichukua rasmi United mwezi Machi 2019 kufuatia kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jose Mourinho.   Ameiongoza Manchester

Continue Reading →

Sancho atambulishwa rasmi Manchester United

Manchester United imemtangaza rasmi winga wao mpya Jadon Sancho kuwa mchezaji wao ikiwa ni takribani wiki mbili tangia usajili wa ada ya pauni milioni 73 kukamilika kutokea Borrussia Dortmund kutua viunga vya Old Trafford.   Baada ya kutambulishwa amesema kujiunga na Manchester United ni sawa na kutimiza ndoto zake. Amehamia Kaskazini Magharibi ya England baada

Continue Reading →

Son ajifunga Tottenham Hotspur miaka minne

Winga wa Tottenham Hotspur Son Heung-min ameingia kandarasi mpya ya miaka minne kuendelea kukitumikia kikosi hicho mpaka mwaka 2025.   Son, 29, amefunga bao 107 katika mechi 280 tangia alipojiunga na timu hiyo kutokea Bayer Leverkusen mwaka 2015.   Ameitumikia timu ya taifa ya Korea Kusini mechi 93 na kufunga goli 27 katika mashindano mawili

Continue Reading →

Everton yamsajili nyota wa Leverkusen Gray

Everton imekamilisha uhamisho wa winga wa zamani wa Leicester City na Bayer Leverkusen Demarai Gray kwa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya pauni milioni 1.7.   Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ameweka kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja endapo mitatu itamalizika akiwa bado yuko vizuri.   Gray anakuwa mchezaji wa tatu

Continue Reading →

Nyota wa Nigeria ajiunga na Brentford ya England

Brentford imekamilisha uhamisho wa mchezaji wa kwanza baada ya kupanda Ligi Kuu England, usajili huo ni wa nyota wa kimataifa wa Nigeria, anayefahamika kwa jina la Frank Onyeka kutokea klabu ya FC Midtjylland amemwaga wino.   Mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo anajiunga na Brentford kwa kandarasi ya miaka mitano ambapo, fedha za usajili imefanywa

Continue Reading →

Arsenal yakamilisha usajili wa Sambi Lokonga

Arsenal imekamilisha uhamisho wa kiungo kijana wa Ubeligiji aliyekuwa anakipiga kunako klabu ya Anderlecht Albert Sambi Lokonga kwa mkataba wa muda mrefu.   Fedha ya uhamisho haijawekwa bayana mpaka sasa lakini inaaminika kuwa ni pauni milioni 17.2.   Alijiunga na Anderlecht akiwa na umri wa miaka 15 lakini alianza kucheza mechi ya kwanza mwaka 2017

Continue Reading →