Manchester United wamesema hawako tayari kulipa zaidi ya pauni milioni 50 kwa winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho, 20, hilo limedokezwa na viongozi wakubwa ndani ya Manchester. Winga huyo raia wa England anatajwa kurudi katika Ligi Kuu ya EPL akitokea Borrusia Dortmund ambapo United imekuwa ikitajwa kama timu pekee ambayo inawania saini ya staa huyo
