Klabu ya Everton imetoa taarifa rasmi kuwa imepokea kibali kutoka kwa serikali ya Uingereza juu ya kujenga uwanja mpya na sasa baada ya ujenzi huo takribani mashabiki 52,000 watakuwa wanaingia. Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini England imekuwa ikiutumia uwanja wa Goodison Park tangia mwaka 1892 na imekuwa ikitafuta uwanja wake kwa miaka 25 sasa.
