AC Milan ikiwa na wachezaji pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kuonyeshwa kadi nyekundu wamefanikiwa kuibuka kidedea dhidi ya Benevento kwa goli 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A. Franck Kessie aliitanguliza Milan kwa goli lake la njia ya penati kabla ya Sandro Tonali kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumfanyia faulo Artur Ionita.
