Kibu Denis, Kisubi watua Simba kimya kimya

Jeremiah Kisubi na Kibu Denis wameonekana wakifanya mazoezi na kikosi cha Simba chini ya kocha Didier Gomes Da Rosa katika mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam. Kuanza kwa mazoezi hayo kunaashiria kuwa wamekamilisha usajili ingawa umekuwa wa kimya kimya tofauti na ilivyokuwa kwa wachezaji wengine kama Peter Banda, wanajiunga na

Continue Reading →

Haya hapa maneno ya Nugaz baada ya kuachana na Yanga

Muda mfupi baada ya Yanga kuweka wazi kuwa haitaendelea kufanya kazi na aliyekuwa Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz kufuatia mkataba wake kumalizika klabuni hapo, Mhamasishaji huyo ametoa maneno ambayo sawa na kuwaaga mashabiki. Itakumbukwa Leo mchana, Yanga iliweka wazi kuwa ndoa ya miaka miwili na Antonio Nugaz imefikia tamati na haitaendelea kufanya kazi pamoja. Kupitia ukurasa

Continue Reading →

Molinga asajiliwa Namungo FC

Namungo FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo David Molinga akitokea Zambia katika klabu ya Zesco United. Molinga maarufu kama “Papaa” anajiunga na Namungo FC ikiwa ni miaka miwili pekee imepita tangia mchezaji huyo kuondoka Yanga iliyokuwa chini ya kocha Mwinyi Zahera. Namungo imeweka

Continue Reading →

Azam yamsajili Yvan Lionnel Mballa wa Cameroon

Dirisha kubwa la usajili la Tanzania limefungwa rasmi usiku wa kuamkia Septemba Mosi huku Azam ikimaliza usajili huo kwa usajili nyota wa kimataifa wa Cameroon Yvan Lionnel Mballa. Usajili wa beki huyo unakamilika kipindi ambacho klabu hiyo imeendelea kujiweka sawa Zambia kwa ajili ya mashindano ya Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Afrika na Kombe la

Continue Reading →

Simba, Kagera zamalizana na Mhilu

Baada ya usajili wake kuzua sintofahamu kubwa kutokana na klabu mama kudai kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Simba haijafuata utaratibu, hatimaye winga Yusuph Mhilu ni mali ya Simba kufuatia Kagera Sugar (klabu mama) kukiri kumalizana na klabu hiyo. Usajili huo umekamilika baada ya Simba kuweka kitita kirefu cha fedha mezani na

Continue Reading →

Yanga yalazwa hoi na Zanaco, Wiki ya Mwananchi

Yanga imepoteza mchezo wa kirafiki kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanaco ya Zambia, mchezo ambao ulikuwa unahitimisha kilele cha Wiki ya Mwananchi. Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya utambulisho wa wachezaji mbele ya mashabiki 60,000 waliojitokeza dimba la Mkapa. Alianza Heritier Makambo kupachika bao dakika ya 30 akimalizia pasi ya Feisal Salum Fei

Continue Reading →

Jezi Mpya Yanga zatambulishwa, Manara atia neno

Klabu ya Yanga imetambulisha rasmi jezi mpya za msimu mpya wa mashindano 2021/22 zikizinduliwa na mmoja wa wasemaji wa klabu hiyo Haji Sunday Manara baada ya kutambulishwa siku moja akitoka kwa wapinzani wao klabu Simba. Uzi huo wa aina tatu, nyumbani, ugenini na nyingine ya tatu zenye rangi ya njano na kijani wanakusudia kuzitumia jezi

Continue Reading →

Manara wa Simba achukuliwa na mahasimu Yanga

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, aliyewai kuwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Sunday Manara ametambulishwa ndani ya Yanga huku akijinasibu kuanza kufanya kazi kwenye utambulisho wa Jezi kesho Jumatano kabla ya tamasha la Jumapili la Wiki ya Mwananchi. Utambulisho wa Haji Manara umefanyika Leo Jumanne Agosti 24, na Mshauri Mkuu wa klabu hiyo Senzo Mbatha

Continue Reading →

Prisons yanasa wachezaji wawili kutoka Azam

Timu ya Tanzania Prisons imefanya usajili wa wachezaji wawili kutokea klabu kubwa hapa nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao 2021/22. Katika kuimarisha kikosi, Prisons imemsajili kipa Benedict Haule kutoka Azam FC na mshambuliaji Moses Kitandu kutoka Costa Do Sol ya Msumbiji. Mkurugenzi wa Ufundi, Kelvin Fredinand amesema Kitandu ni Mtanzania aliyekuwa

Continue Reading →