Gwambina yawaganda Yanga na kugawana alama

Kikosi cha Yanga Sc kimebanwa mbavu na Gwambina FC kwenye mechi ya Ligi Kuu nchini Tanzania iliyopigwa dimba la Gwambina Complex kwa sare tasa ya 0-0. Yanga ambayo iko chini ya kocha Cedric Kaze baada ya yule wa awali Krmpotick kufutwa kazi, kabla ya mchezo wa leo ilikuwa imeshinda mechi tatu mfululizo (Polisi Tanzania, KMC

Continue Reading →

Mtibwa Sugar yachafua rekodi za Azam FC

Waswahili wanasema ukimuona tembo juu ya mti ujue ni suala la muda tu yule tembo kuwa chini, ndicho unaweza kulinganisha na tukio la Azam Fc kupoteza mechi ya ugenini dimbani Jamhuri ya Morogoro kwa mara ya kwanza. Azam ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara, wamekutana na kisiki cha mpingo baada ya kupoteza mchezo wao

Continue Reading →

Simba wapapaswa na Ruvu Shooting 1- 0 dimba la Uhuru

Ruvu Shooting imetoa adhabu nyingine kwa Simba na kutonesha kidonda cha pale wanajeshi wa magereza walipokitengeneza wiki iliyopita. Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Tanzania wanakutana na kipigo cha pili mfululizo kwa mara ya kwanza tangu walipolichukua taji kutoka kwa Yanga baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo, walianza na Tanzania Prisons na

Continue Reading →

Tanzania Prisons yamlaza hoi mnyama Simba

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Tanzania Simba SC wamekutana na kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons mtanange wa Ligi Kuu nchini Tanzania VPL uliopigwa dimba la Nelson Mandela Sumbawanga, Rukwa. Bao pekee katika mechi hiyo iliyotawaliwa na nguvu limewekwa nyavuni na mshambuliaji wa Wajelajela Original Samson Mbangula kunako kipindi cha pili dakika

Continue Reading →

Simba yatua Sumbawanga kuwawinda Tanzania Prisons

Kikosi cha Simba leo kimetua katika ardhi ya Sumbawanga, Rukwa ambako kitakuwa na mchezo wa Ligi Kuu nchini Tanzania utakaopigwa dimba la Nelson Mandela mkoani humo siku ya Alhamis Octoba 22. Mabingwa hao watetezi walianza safari ya kuelekea Rukwa mara baada ya kumaliza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege Fc ya Zanzibar lakini walikuwa na

Continue Reading →