Licha ya ahadi kibao, Ihefu yashuka daraja

Ng’ombe hanenepi siku ya mnada, kauli ambayo inaweza kuwa sawa na mipango ya kikosi cha Ihefu kutoka Mbeya ambacho kiliweka mipango lukuki kipindi cha mwishoni kabisa mwa Ligi badala ya kuanza mapema kabisa jambo ambalo lilifanya ng’ombe akashiba na si kunawiri na kunenepa.   Imeshuka daraja msimu huu baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0

Continue Reading →

Bocco wa Simba kinara upachikaji mabao VPL

Nahodha wa klabu ya Simba John Raphael Bocco amewapongeza wachezaji wenzake ndani ya klabu hiyo kwa ushirikiano aliopata hasa kutoka kwa washambuliaji Medie Kagere na Chris Mugalu.   Bocco amesema ulikuwa msimu bora kwao kama washambuliaji pamoja na wachezaji wote na kila aliyepata nafasi alifunga na ni moja ya chachu iliyosababisha ubingwa wa msimu huu.

Continue Reading →

Yanga yagawana alama na Dodoma Jiji

Yanga imegawa alama moja nayo akichukua moja na kuiacha moja dimba la Jamhuri Dodoma kutokana na sare tasa katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Leo Jumapili Julai 18.   Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imepata pointi hiyo katika kipindi ambacho inajiandaa na mchezo muhimu wa Kombe la FA dhidi

Continue Reading →

Simba wasema ubingwa ni matokeo ya Uwekezaji

Simba imekabidhiwa taji la Ligi Kuu Bara baada ya kukamilisha mzunguko wa pili kwa msimu wa 2020/21 kwa ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Namungo Fc mtanange uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa. Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha alama 83 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile. Namungo inabaki na pointi zake 43 na msimu

Continue Reading →

Kabumbu ya VPL 2020/21 kufikia tamati Jumapili

Ligi Kuu Tanzania Bara inafikia ukomo Leo Jumapili Julai 18 kwa timu zote 18 kushuka dimbani katika viwanja mbalimbali kuwania alama tatu na nyingine kukamilisha ratiba kufuatia kuvuna lengo hitajika kwa msimu wa 202/21.   Wakati Ligi ikifikia tamati, bingwa ameshapatikana ambaye ni Simba Sports Club ikiwa ni mara ya nne mfululizo, Simba ambayo itashuka

Continue Reading →

Bocco, Gomes wakimbiza tuzo binafsi VPL

John Raphael Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, huku kocha Didier Gomes wa timu hiyo akichaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi huo. Bocco ambaye ni nahodha wa Simba na Gomes wametwaa tuzo hizo baada ya kuwashinda wenzao waliongia nao fainali kwa mwezi Juni katika uchambuzi

Continue Reading →

Niyonzima awaliza mashabiki Yanga, Ihefu waomba “Poo”

Pengine usemi wa kitu hakionekani kuwa na thamani mpaka kitoweke ndiyo imedhihirika katika kandanda ya Yanga na Ihefu baada ya dakika 90 kukamilika na Haruna Hakizimana Niyonzima kuchukua kipaza sauti na kusema viongozi kwakherini, wadau kwakherini, na mashabiki kwakherini. Kutaja tu neno mashabiki, baadhi yao mwenye roho nyepesi walijikuta “automatic” machozi yakiwalenga na kuwatoka wakiwa

Continue Reading →