Cavani karibuni kumwaga wino Man United

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Edinson Cavani yuko mbioni kuongeza kandarasi mpya ya kuendelea kusalia Manchester United kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Cavani, 34, alijiunga na Manchester United kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Paris St-Germain Octoba kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba mpya wa miezi 12.

Inafahamika kuwa mchezaji huyo anatamani kuondoka England na kwenda nyumbani Uruguay au Argentina lakini Bosi wake Ole Gunnar Solskjaer amesema anahitaji kuona Strika huyo anabakia Old Trafford.

Ole amesema anamatumaini ya kumuona Cavani akisalia klabuni hapo kutokana na umuhimu wake kwa wachezaji wenzake mbali na uwezo wake mkubwa wa upachikaji mabao.

Klabu ya Boca Juniors ya Argentina imekuwa ikuhusishwa kumsajili mshambuliaji huyo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares