Ceballos arudi tena Emirates na kujiunga na Arsenal kwa mkopo

Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid ambaye msimu uliopita alikuwa anakipiga kunako klabu ya Arsenal Dani Ceballos alikuwa amerejea Madrid lakini sasa imethibitika kuwa amejiunga na The Gunners kwa mkopo wa msimu mzima baada ya kushindwa kumshawishi Zinedine Zidane.

Akiwa Arsenal kwa msimu uliopita alikuwa kwenye kiwango bora ingawa bado kocha Zinedine Zidane hajaridhishwa na kiwango chake na kuendelea kumtazamia akiwa sehemu nyingine atakayopata nafasi ya kucheza.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na Real Madrid akitokea Real Betis mwaka 2017, msimu uliopita alicheza mechi 37 akiwa na Washika Mtutu hao wa London.

“Dani ni sehemu yetu, alikuwa muhimu kwetu msimu uliopita” alisema kocha wa Arsenal Mikel Arteta.

“Nampenda Dani kwa hali yake,  anajituma, ni mbunifu sana jambo litakalotupa nguvu kama timu kuwa nae”.

Author: Asifiwe Mbembela