CECAFA yatoa ratiba ya michuano ya U20

Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na kati CECAFA limetangaza droo ya michuano ya mwaka huu kwa vijana kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 inayotarajiwa kuanza Novemba 22 hadi Desemba 2 Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Wenyeji Tanzania, wamepangwa katika kundi la A na Somalia na Djibouti. Kundi B kuna Burundi, Sudan Kusini na Uganda huku kundi likiwa na Kenya, Ethiopia na Sudan.

Author: Kaka Abuso

Sharing is caring!

0Shares