Chama cha soka Ujerumani chasema Loew atabaki kuwa kocha wa Ujerumani katika Euro 2020

Joachim Loew atabaki kuwa kocha wa Ujerumani katika mashindano ya Euro 2020 licha ya kichapo cha fedheha cha wiki iliyopita, rais wa Chama cha Soka Ujerumani – DFB amesema katika mahojiano leo.

Loew yuko chini ya shinikizo baada ya Ujerumani kufungwa 2 – 1 nyumbani dhidi ya Macedonia Kaskazini katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia, miezi minne baada ya kichapo cha 6-0 na Uhispania katika Ligi ya Mataifa.

Ujerumani wanapambana kupata muendelezo mzuri tangu walipomaliza wa mwisho katika kundi lao la Kombe la Dunia 2018 chini ya Loew, wakati wakiwa mabingwa watetezi.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61, anatarajiwa kubwaga manyanga baada ya miaka 15 usukani kufuatia mashindano yaliyocheleweshwa ya Ubingwa Ulaya kuanzia Juni 11 hadi Julai 11. Rais wa DFB Fritz Keller ameliambia gazeti la kila siku la Bild kuwa mechi ya kukatisha tamaa dhidi ya Macedonia Kaskazini haijabadilisha kitu kuhusiana na mipango yao. ”Jogi Loew na timu yake watatathmini kila kitu na kuweka mapendekezo mwafaka ya kupata mafanikio katika mechi za Euro.” Amesema Keller

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares