Chamberlain aurefusha mkataba na Liverpool

Staa wa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain ameongeza mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo sasa mpaka 2023. Alijiunga na Majogoo wa Jiji la Liverpool mwaka 2017 akitokea Arsenal.

Alex, 25, amerejea mwezi Aprili baada ya kushindwa kucheza mwaka mzima kwa sababu ya majeraha aliyoyapata katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya AS Roma mwaka 2018.

Mchezaji huyo mwenye uraia wa England akiwa ameichezea mechi 32, awali mkataba wake ungeisha mnamo mwaka 2022.

“Nimefurahia kusaini mkataba mpya,” alisema.  “Huenda nikawa na msimu mzuri na kurudisha fadhira za kutocheza msimu uliopita”.

Oxlade-Chamberlain alianza kuitumikia Liverpool mwaka 2018 dhidi ya Southampton akicheza dakika 89, akicheza pia dakika 45 kwenye mchezo wa Agosti 14 dhidi ya Chelsea katika mashindano ya Super Cup.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends