Chelsea, Man United mchekea kundi lake Uefa, PSG ngumu na Man City

Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imetolewa rasmi Leo Alhamis Agosti 26, ambapo Mabingwa wa Ligi hiyo klabu ya Chelsea watacheza na miamba ya soka la Italia Juventus wakati matajiri wa Jiji la Paris, Paris St-Germain wakicheza na Manchester City.

Mtiririko mzuri wa droo hiyo uko hivi; Manchester City itachuana vikali na RB Leipzig, Paris St-Germain na Club Brugge Kundi A, wakati Chelsea ikiwa kundi moja la H na Juventus, Zenit St Petersburg na Malmo.
Wakati huo, klabu ya Mashetani Wekundu Manchester United itacheza na Villarreal, Atalanta na Young Boys kutoka Switzerland kundi F.
Liverpool wako kundi moja na Atletico Madrid, Porto na AC Milan kundi B.
Kundi C: Sporting Lisbon, Borussia Dortmund, Ajax, Besiktas
Kundi D: Inter Milan, Real Madrid, Shakhtar Donetsk, Sheriff Tiraspol
Kundi E: Bayern Munich, Barcelona, Benfica, Dynamo Kyiv
Kundi G: Lille, Sevilla, FC Salzburg, Wolfsburg
Group H: Chelsea, Juventus, Zenit St Petersburg, Malmo
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu itachezwa Urusi Jumamosi ya Mei 28 dimba la St Petersburg.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares