Chelsea, Villarreal kupepetana vikali Agosti 11 mjini Belfast mchezo wa UEFA Super Cup

Mchezo wa Uefa Super Cup baina ya Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Chelsea dhidi ya Mabingwa wa Ligi ya Europa Villarreal utachezwa Agosti 11 katika mji wa Belfast, Ireland Kaskazini.
Istanbul awali ilipangwa kuwa mwenyeji wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya UEFA kuhamisha mchezo huo mpaka Porto nchini Ureno kutokana na vizuizi vya Covid-19 vilivyokuwepo katika taifa hilo.
Chama cha Soka Uturuki kimesema kuwa fainali hiyo itapigwa dimba la Windsor Park mjini Belfast, katika tarehe tajwa.
“Tumefarijika kuambiwa Uefa wamethibitisha kuwa mchezo utachezwa Belfast, alisema Mtendaji Mkuu wa FA ya Uturuki.
Hata hivyo, bado mpangilio mzuri baina ya klabu husika na mashabiki haijakaa sawa, inaelezwa itatangazwa baadaye.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares