Chelsea waididimiza Fulham EPL, Havertz ajibu pigo

Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Kai Havertz alifunga goli mbili dhidi ya Fulham katika ushindi wa 2 – 0 na kuweka sawa mazingira ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao 2021/22.

Havertz, alikuwa miongoni mwa wachezaji watano ambao walipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza tofauti ya kile ambacho kilianza dhidi ya Real Madrid mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bao la Havertz lilikuja akimalizia pasi ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa England Mason Mount kabla ya kukwamisha mpira nyavuni akitumia vyema mpira wa winga wa Ujerumani Timo Werner.

Fulham walipata nafasi ungwe ya kwanza kupitia Antonee Robinson na Ola Aina lakini juhudi hizo ziliishia mikononi mwa mlinda mlango Edouard Mendy.

Chelsea, ambao wanahitaji ushindi au sare tasa kwenye mechi ya mkondo wa pili dhidi ya Real Madrid kufuzu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,  wanaendelea kujiweka kando na wapinzani wao West Ham United.

“Kai tunajua ni mchezaji bora, si ajabu kushindwa kufanya vizuri msimu wa kwanza”, alisema Thomas Tuchel kocha wa Chelsea.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares