Chelsea yaambulia pointi moja kwa Southampton baada ya sare ya 1-1

Kocha wa klabu ya Southampton Ralph Hasenhuttl amesema Ana matumaini kuwa kupata alama moja mbele ya Chelsea na kuhitimisha mfululizo wa vipigo kwa klabu yake kunaweza kuirejesha kwenye ushindani baada ya kupoteza mechi sita mfululizo za EPL.

Kocha Ralph anayasema hayo baada ya kikosi chake kutoa sare ya goli 1-1 na The Blues kwenye mchezo uliopigwa Leo Jumamosi.

Wenyeji Southampton walichukua uongozi kupitia kwa nyota wao wa klabu ya Liverpool Takumi Minamino akimalizia mpira wa Redmond.

Hata hivyo chelsea walirudi na kupata goli kwa njia ya penati iliyofungwa na Mason Mount baada ya Danny Ings kumwangusha Mount mwenyewe eneo la hatari.

Licha ya matokeo ya sare, kocha wa watakatifu Southampton ameridhika nayo akiamini ni hatua kubwa kwake na timu yake.

Alama moja inaiacha Chelsea nafasi ya nne na pointi 43 kwenye msimamo wa EPL wakati Southampton wakiwa nafasi ya 13 na alama 30..

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares