Chelsea yafuzu Champions League baada ya kuitandika Watford

55

Chelsea wamejikatia tiketi ya kucheza kandanda la Champions League msimu ujao baada ya kupata ushindi dhidi ya Watford dimbani Stamford Bridge.

Ushindi ukichanganya na sare ya Arsenal dhidi ya Brighton, una maana kuwa The Blues wamejihakikishia nafasi ya kumaliza katika nne bora kwenye Ligi ya Premier.

Baada ya kipindi kigumu cha kwanza, Chelsea walifunga mabao mawili katika dakika tatu mapema katika kipindi cha piili kupitia mabao ya kichwa ya Ruben Loftus-Cheek and David Luiz. Gonzalo Higuain alihakikisha kuwa vijana hao wa kocha Maurizio Sarri wanapata pointi zote tatu kwa kufunga bao lake la tano msimu huu katika klabu hiyo.

Ushindi huo umeiweka Chelsea katika nafasi ya tatu, pointi moja mbele ya Tottenham na nne mbele ya nambari tano Arsenal.

Author: Bruce Amani