Chelsea yagawa alama na mabingwa wa Europa League Sevilla

Chelsea imelazimishwa kugawa alama na mabingwa wa Ligi ya Europa Sevilla katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Uefa uliopigwa dimba la Stamford Bridge ukimalizika kwa sare tasa. Kocha Lampard akiwa anaiongoza Chelsea katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Ulaya msimu huu amejikuta akitawala na wageni hao kwa dakika nyingi za mchezo.

Kukiwa na nafasi chache za wazi katika mtanange huo, kipa namba moja wa Chelsea Edouard Mendy aliyerudi langoni baada ya kukosekana kwenye mtanange wa wikiendi alikuwa na kazi ndogo hasa ya kusevu mpira wa Nemanja Gudelj.

Matokeo hayo si mabaya kwa timu hizo kwani ndio kwanza ratiba ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeanza rasmi leo Jumanne katika msimu huu mpya.

Author: Bruce Amani