Chelsea yagawana alama na Arsenal

Arsenal wametoka nyuma goli 1-0 wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2 dhidi ya Chelsea mtanange wa Ligi kuu ya England uliopigwa leo dimba la Stamford Bridge.

Arsenal ilimkosa mlinzi wa kati David Luiz aliyeonyeshwa kadi nyekundu kuanzia dakika za awali ngwe ya kwanza mpaka walipopata nguvu ya kushinda na vyema.

Vijana wa Mikel Arteta, The Gunners walionekana kama wangepokea kipigo kizito kutoka kwa Chelsea baada ya Luiz kuonyeshwa kadi kisha Jorginho akafungua ukurasa wa magoli kwa penati na la pili likafungwa na nahodha Cesear Azipiliqueta.

Goli la kwanza  la Arsenal limefungwa na Martinelli na akifuatiwa na Hector Bellirian ambaye ndiye aliyeipa alama moja Arsenal ambayo muda mwingi wa mchezo huo iliutumia kwa kujilinda.

Matokeo hayo yanaifanya Chelsea kuendelea kusalia nafasi ya tano ya ligi kuu ya England wakati Arsenal ikiwa nafasi ya 10 alama 30 katika michezo 24.

KIPI KIFUATACHO

Chelsea itakutana na Hull Cify iliyopo ligi daraja la England hatua ya nne ya FA wakati Arsenal ambayo pia ipo kwenye mbilinge hizo itacheza na Bournemouth siku ya Jumapili.

Matokeo mengine EPL leo Jumanne.

Sheffield United 0-1 Manchester City

Everton 2-2 Newcastle United

Aston Villa 0-1 Watford

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends