Chelsea yaibamiza Leicester 3-0 EPL

Vinara wa Ligi Kuu England Chelsea imeibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa kandanda ya ligi na kuendelea kutengeneza mazingira ya kutawala nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa EPL.

Chelsea imevuna alama hizo tatu, kwenye mechi iliyopigwa dimba la King Power ambapo magoli ya Chelsea yakifungwa na mlinzi wa kati wa Ujerumani Antonio Rudiger akifunga kwa kichwa, kiungo mkabaji N’Golo Kante na Christian Pulisic ambaye linakuwa bao la kwanza baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeruhi.

Majaribio ya nguvu kwa Leicester City yalitokea wakati mlinda mlango Edouard Mendy alifanya sevu nzuri kukataa magoli ya mchezaji wa Ghana Daniel Amartey na kichwa cha Jamie Vardy.

Ushindi huo unaifanya Chelsea kutengeneza tofauti ya alama sita kileleni na timu iliyonafasi ya pili Liverpool ingawa utofauti unaweza kujitokeza kama Liverpool itashinda dhidi ya Arsenal.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends