Chelsea yaibuka kutoka kwenye kipigo, yaichabanga Porto 2-0 Ligi ya Mabingwa

Chelsea imeibuka vyema kutoka kwenye kichapo cha goli 5-2 dhidi ya West Bromwich Albion mtanange wa EPL na kushinda bao 2-0 dhidi ya FC Porto mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali uliopigwa Leo Jumatano.

Magoli ya Chelsea yamefungwa na Mason Mount kipindi cha kwanza na kumpa ahueni kocha Thomas Tuchel, ambaye alikutana na wakati mgumu baada ya sintofahamu ya beki wa kati Antonio Rudiger na kipa Kepa Arrizabalaga.

Ben Chilwell aliongeza bao la pili katika mechi hiyo, kufuatia makosa ya Corona baada ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Marekani Christian Pulisic mpira wake kugonga mtambaa wa panya

Mechi zote mbili nyumbani na ugenini zinachezwa katika uwanja wa Sevilla unaofahamika kama Ramon Sanchez Pizjuan kutokana na athari ya Covid-19 na vizuizi vya kusafiri kwa mataifa mengi barani Ulaya.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares