Chelsea yaipa kipigo Norwich City, yaichapa 7-0

Kocha Thomas Tuchel ameendelea kuwa bora tangia atue Chelsea akitokea Paris St-Germain na kutwaa ubingwa kwenye msimu wake wa kwanza wa Uefa, ubora huo unaochagizwa na kipigo kizito cha goli 7-0 walichokitoa kwa Norwich City.

Kiungo mshambuliaji wa England Mason Mount amefunga goli tatu (hat-trick) kabla ya Callum Hudson Odoi, Reece James, Ben Chilwell wote kufunga goli moja moja na mlinzi wa pembeni Max Aaron kujifunga goli.

Norwich City wakiwa ugenini katika dimba la Stamford Bridge waliendelea kupata wakati mgumu tena baada ya mlinzi Ben Gibson kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Matokeo hayo yanaifanya Norwich City kubakia kwenye mstari wa mwisho wa msimamo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends