Chelsea yainyakua saini ya Timo Werner kutoka RB Leipzig

Klabu ya Chelsea imekamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig Timo Werner.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amekuwa akitajwa kwenda kunako klabu ya Liverpool kwa muda sasa na tayari ameshasema kuwa anafurahi kuhusishwa huko, hata hivyo Liverpool inaonyesha haitamsajili tena.

Ripoti zinaonyesha Werner ana kipengele kinachomruhusu kuondoka klabuni hapo kwa dau la Euro milioni 54. Wakati Werner anahusishwa tayari Olivier Giroud aliongezwa mkataba mpya wa mwaka mmoja na Chelsea mwezi uliopita.

Werner, amefunga goli 11 kwenye mechi 29 kwa timu ya taifa, Chelsea ikikamilisha dili hilo utakuwa usajili wa pili wa The Blues baada ya winga wa Ajax Hakim ziyech kujiunga nayo mwezi Februari.

Mwezi wa kwanza, Kocha Mkuu wa Chelsea Frank Lampard alikuwa katika ushawishi wa washambuliaji wawili mosi ni strika wa PSG Edinson Cavani na Dries Mertenes wa Napoli ingawa hakuna dili lolote lilitoa mwanga kama hili.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends