Chelsea yapata ushindi dhidi ya Reading mechi ya kujipima

Chelsea imeibuka na ushindi dhidi ya Reading wa goli 4-3 katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu ujao wa mashindano.

Kinda wa Chelsea Mason Mount amefunga goli 2 huku akionyesha kiwango bora chini ya kocha mpya Frank Lampard.

Chelsea ikitoka kushinda mchezo dhidi ya Barcelona walijikuta wakitanguliwa na Reading kupitia goli la Josh Barrett kabla ya Ross Barkley kusawazisha kwa mpira wa kutengwa kisha Kennedy akafuta matumaini ya kushinda kwa Reading.

Mbali na goli la Barrett, goli nyingine za Reading zimefungwa na Michael Morrison pamoja na Sam Baldock.

Baada ya ushindi wa leo, Chelsea imebakiwa na michezo miwili ya kirafiki kabla ya kufikia Agosti 11 itakapocheza na Manchester United Old Trafford mchuano wa EPL, michezo yenyewe ni ule Borrusia Monchengladbach na Red Bull Salzburg.

Katika mechi nyingine za kirafiki, Liverpool walilamba 3 – 0 dhidi ya Napoli wakati Arsenal wakifungwa 2 – 1 na Olympique Lyon katika dimba la Emirates na kubeba Kombe la Emirates

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends