Chelsea Yapokea Kipigo Tena
Kocha Frank Lampard ameendelea kupokea vipigo kwenye wadhifa wa kuisimamia klabu ya Chelsea mpaka mwisho wa msimu kwani amekubali kufungwa bao 2-1 dhidi ya Brighton Hove Albino mchezo wa EPL uliochezwa dimba la Stamford Bridge Jumamosi.
Chelsea wakiwa wametoka kutweta na maumivu ya kufungwa na Real Madrid bao 2-0 mchezo wa Uefa walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Conor Gallagher akimalizia pasi ya Mudryk.
Hata hivyo, Brighton walifunga magoli yake kupitia kwa Danny Welbeck lililomuwa ni bao la kusawazisha na mchezaji kinda wa akiba Julio Enciso.
Kwa matokeo hayo, Chelsea inashika nafasi ya 11 wakati Brighton wamepanda daraja kidogo na kushika nafasi ya 7.
