Chelsea yavuta Mido ya Mpira ya Atletico Madrid

Chelsea imemsajili kiungo mkabaji wa kimataifa wa Hispania na Atletico Madrid Saul Niguez kwa mkataba wa mwaka mmoja kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja.

Niguez 26, alikuwa mchezaji mhimili kwenye kikosi cha Atletico Madrid ambacho kilishinda ubingwa wa La Liga msimu uliopita ambapo alicheza jumla ya mechi 33.

Awali ilikuwa inadhaniwa kuwa Chelsea wasingeweza kumsajili kiungo huyo kutokana na kuchelewa kuanza mazungumzo kwani nguvu kubwa ziliwekezwa kwa beki Jules Kounde wa Seville

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares