Chilwell kuwa nje ya Chelsea wiki sita

39

Beki wa kushoto wa Chelsea Ben Chilwell atakuwa nje ya uwanja kwa sababu ya majeruhi ya goti kwa angalau wiki sita akiuguza majeraha yake ambayo anaweza asifanyiwe vipimo vya afya.

Mchezaji huyo wa zamani wa Leicester City mwenye umri wa miaka 24, alipata maumivu hayo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus ambapo Chelsea ilishinda bao 4-0.

Kocha wa kikosi hicho, Thomas Tuchel amethibitisha hilo ambapo amesema kuwa baada ya wiki sita tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuona maendeleo yake.

“Tunaamini wiki sita kwa sababu hata ukiangalia mwili wake hauonyeshi kama anashida kiasi hicho”.

Chilwell ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye ubora mkubwa ndani ya The Blues msimu huu ambapo amekuwa akitumika kama “Wing Back” kwenye mfumo wa 3-5-2.

Author: Bruce Amani