Chui avamiwa Mlima Kenya, Gor yaendelea kupanda

226

Kwa Ingwe we acha tu, Gor nayo wueh!!! Huku mashabiki wa AFC Leopards wakilia na kusaga meno kuhusu matokeo mabovu ya timu yao, watani wao Gor Mahia wameshika laini!

Ingwe ilipigwa 2-1 na Mount Kenya United Jumatano uwanjani Machakos huku Kogalo ikimliza mwenyeji Vihiga United 1-0 uwanjani Bukhungu shukrani kwa bao lake Nicholas Kipkirui.

Sasa ipo hivi, baada ya straika wa zamani wa Ingwe John “Softie” Ndirangu kufungua nyavu za Ingwe dakika ya 30, beki Abdallah Salim alisawazisha kabla ya mapumziko huku Timonah Wanyonyi akiwahi la ushindi kipindi cha pili.

Kocha mpya wa Leopards amekaribishwa na kichapo

Hawa ni Ingwe waliopigwa 4-1 na Bandari siku ya Jumapili, hii ni Ingwe moja iliyomwajiri kocha wa tatu msimu huu, Mnyarwanda Andre Cassa Mbungo akitia wino kwenye mkataba wa mwaka mmoja na nusu. Hii ni Ingwe moja iliyomtema Mserbia Marko Vasiljevic aliyeelekea kwao nyumbani wakati Mbungo anamwaga wino kwenye mkataba leo mwendo wa saa tano kabla ya kuelekea Machakos kuchinjwa.

“Timu haina motisha ndicho cha kwanza nakileta kisha basi, tutajikwamua,” alisema Mbungo.

Isitoshe, mashabiki walimnzingira nahodha Robinson Kamura baada ya mechi wakitaka majibu ya kwa nini matokeo si mazuri?

Mashabiki wa Leopards wanadai majibu kutokana na matokeo mabaya

“Hatuna straika, sijui viongozi malengo yao huwa nini mie nafikiri timu yeyote duniani inayotaka ushindi humwaga mihela kuwahi straika lakini tangu tumpoteze Ezekiel Odera, hatuna mwingine,” alihamaki Kamura akizingirwa na umati wa mashabiki wa Ingwe.

Kamura yungali na mshtuko kama beki kivipi ndiye mfungaji bora kwa magoli manne kwenye mabingwa hao mara 13 wa KPL kama Leopards? Akili kichwani mwa uongozi uliopata pigo baada ya mechi alipotangaza kujiuzulu naibu katibu mkuu Stazo Omung’ala.

Jedwali linakaa hivi! Gor wapo nafasi ya tatu kwa pointi 19 huku Ingwe ikiwa nafasi ya 15 kwa pointi 10.

Kule Kisumu, Western Stima iliandikisha ushindi wa 1-0 dhidi ya Zoo Kericho.

Patachimbika nguo kuchanika Jumamosi hii Gor ikimwalika Leopards kwenye mashemeji debi ya kwanza mwaka huu

Author: Vincent Stephen